Monday, June 21, 2010

Lilikuwa ni tukio la muda mfupi tu

tukio la "Mlima kuachia" ni tukio ambalo huchukua muda mfupi sana. Kwa siku hii (Juzi) tukio hili lilichukua muda usiozidi dakika 5 na baada ya hapo Kibo ilimezwa na mawingu. Ndio maana wenyeji wangu walipoona umeachia, haraka walinijulisha na kuniambia nifanye haraka ili niweze kupata taswira chache kwa ajili ya wadau wa TembeaTz.

Haukupita muda mrefu (nadhani kama dakika 2 hivi) mawingu yalianza kuufunika mlima. Nilipomuuliza mwenyeji wangu kama utaachia tena akanijibu "Ahh.. hiyo ndio mpaka kesho, napo pia ni kwa kubahatisha".

Baadae Kilele cha Kibo kilipotea kabisa na kufunikwa na mawingu. Nilisubiri kwa muda kadhaa ili kuona kama utaachia tena lakini hali haikubadilika. Wingu lilizidi kuufunika kabisa.

Kuna sehemu ambazo wenyeji wa Kibosho wanazijua ambapo unapata view kali zaidi ya kilele cha Kibo mlima ukiwa umeachia. Kwa siku hii hatukuweza kwenda hapo kwani wenyeji waliniambia mpaka tukifika mahali hapo, Kilele kitakukuwa kimefunikwa na mawingu na itakuwa ni kazi bure. Hayo ndio maajabu ya mlima..

No comments:

Post a Comment