Sunday, June 6, 2010

mandhari maridhawa, bwawa la Ranzi..

ndinga ikichanja mbuga na wageni kuelekea lilipo bwawa la Ranzi ili kujionea mandhari maridhawa ya huko.

Full kujiachia...

eneo lililopo pembezoni mwa bwawa hili hutoa fursa ya wageni kufanya shughuli mbalimbali wanapotembelea eneo hili.

Anayeamua kuota jua sawa... anaeamua kushangaaa maji ktk bwawa ambalo lipo milimani sawa... yote hii ikiwa ni namna ambazo mgeni anaweza kuliwaza akili yake akiwa pembezoni mwa bwawa la ranzi huko milima ya pare ya Kusini (Mbaga), Same, Mkoani Kilimanjaro

Watu waliosoma shule ijulikanayo kama shule ya Manka iliyopo huko Milima ya Mbaga Same wanapaelewa sana hapa mahali. Inaelezwa ya kwamba hapa ndio moja ya picnic site zao madenti wa Shule ya sekondari ya Manka. Ahsante ya picha kwa mdau Elly Kimbwereza wa Tona Lodge iliyoko huko Mbaga, Same.

No comments:

Post a Comment