Sunday, June 6, 2010

Mandhari maridhawa, nje ya Ngorongoro Crater...

Taswira hizi zinakuonyesha sehemu ya safari kati ya gate la crater mpaka kufika lango la kuingia ndani ya crater. Mdau huo mlima hapo hakuna cha adobe wala photoshop... picha ipo kama hali halisi ilivyo..

Ngorongoro ni eneo ambalo kuna milima kadhaa, huu ni mmojawapo ambao upo pembeni kidogo ya crater.

Mwaka jana nilipokuwa huko kulikuwa na nyumba za wananchi jamii ya wamasai wakiwa nje ya crater lakini ndani ya eneo la hifadhi. Kushoto ni baadhi ya boma/nyumba za wamasai. Crater yenyewe ipo kulia mwa hiyo barabara uionayo. Hii barabarani itakupeleka mpaka ktk gate la kuingilia crater na ukiendelea nayo utakuwa unaelekea hifadhi ya taifa ya Serengeti na Mkoa wa mara kwa ujumla.

Eneo la wazi unaloliona kwa mbali ndio uwanda wa hifadhi ya Serengeti. Barabara unayoiona pembezoni mwa huo mlima hapo kati ndio inayoelekea hifadhi ya taifa ya Serengeti baada ya kupita Ngorongoro crater.

picha zote ni toka ktk maktaba ya TembeaTz

No comments:

Post a Comment