Sunday, June 6, 2010

Wanapatikana Zanzibar tu

Kutokana na ukweli ya kwamba mbega hawa wanapatikana huko kisiwani Unguja pekee, wamepewa jina la Zanzibar Red Colobus (mbega wekundu wa Zanzibar). Wanapatikana zaidi ktk ile hifadhi maarufu huko visiwani ijulikanayo kama Jozani.

Wanaitwa mbega wekundu kutokana na rangi nyekundu iliyopo mgongoni mwao.

Mdau JSK aliyekuwa kisiwani Unguja kikazi siku chache zilizopita, alitembelea msitu wa Jozani na kutumwagia picha za Mbega wekundu wa Zanzibar na mambo mengine kibao yanayopatikana ndani ya msitu wa Jozani. Shukran sana kwa mdau JSK kwa taswira hizi na nyinginezo ambazo Tembeatz imezipata.

No comments:

Post a Comment