Thursday, June 17, 2010

Mto Seronera, Serengeti NP

Kwa wale wanaopenda kufuatilia habari za migration ya wanyama kule Serengeti, mto Mara ndio mto ambao watakuwa wanauelewa vizuri. Migration inapofika ktk mto Mara, nyumbu wengi hufa kwa kuliwa na mamba au kuzama kwa kushindwa kuogelea. ni namna moja ambayo mizani ya nature inaji-balance ktk hifadhi hii.
Ukiachia mto Mara, Serengeti kuna mto mwingine ujulikanao kama mto Seronera. Mto huu upo maeneo ya katikati ya Hifadhi ya Serengeti. Ukiwa maeneo ya Seronera huatakosa kuuvuka mto huu. Ukiwa ktk game drive maeneo haya unaweza kuuvuka mara kadhaa ktk pita pita zako. Sio mto mkubwa kama mto Mara lakini maji yake yanahifadhi viboko kadhaa na kutoa mandhari maridhawa ktk baadhi ya sehemu utakapokutana nao.

Huu ulikuwa ni upande mmoja wa Barabara.

huu ulikuwa ni upande wa pili wa mto. Gari letu lilikuwa limesimama juu ya culvert/daraja

Egyptian geese. Siku hii tulikuwa njiani kwenda kwenye bwawa la viboko lijulikanalo kama Retima hippo pool lililopo ktk Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. picha zote toka ktk maktaba ya TembeaTZ

No comments:

Post a Comment