Masikio ni mmoja ya wanyama wa porini ambae anaelezewa kuwa ni mwerevu sana kushinda wanyama wengine. Werevu huu unakuja kutokana na ukweli wa kwamba masikio ana uwezo mkubwa wa kukumbuka vitu na matukio fulani fulani. Juu ya hapo masikio ana uwezo mkubwa wa kusikia hata sauti ndogo na kujua inatokea wapi na kisha yeye kuamua akimbie au apambane nayo. Hapo usiweke pembeni uwezo wake wa kunusa. Hivi ni baadhi ya vipengele vinavyomuweka masikio mbele ya adui yake au hata mbele ktk mashindano ya kupata msosi kwa jamii yake. Licha ya mahitaji yake ya chakula kuwa ni makubw, lakini ukame ukifika kundi la tembo litatembea maili nyingi kwenda kule ambako linaamini kuwa hawatakosa chakula. na ukweli ni kwamba huwa hawakosei.
Inaelezwa ya kwamba uwezo wa masikio kukumbuka vitu mbalimbali ndio umemfanya mnyama huyu aweze kuishi na kushinda mabadiliko mbali mbali ambayo wanyama wengine ilibidi wayapitie ili kwenda sambamba na muda. Wanyama wengine ndio huwa wa kwanza kuangamia njaa inapoingia ktk pori kutokana na kutojua waende wapi kupata chakula kipindi cha ukame.
Endapo kundi la tembo likapita mahali (nje ya hifadhi) na kukuta kuna chakula au maji, hasa hasa wakati wa kiangazi/ukame, basi ni dhahiri kundi hilo litarudi tena siku nyingine endapo hali ya chakula itazidi kuwa mbaya. Wataalam wanaenda mbele na kusema ya kwamba endapo atapata upinzani mkali utakaotishia maisha yake, basi tembo huyo hatopita tena njia hiyo kwa kuhofia yale yaliyomkuta awali. Purukushani ile itakuwa ni fundisho ambayo tembo huyo hataisahau na kamwe kama atakuwa ktk kundi ambalo litakuwa likielekea upande ule, ni dhahiri atawaashiria wenzake kuwa huko siko na watatfuta njia nyingine.
ktk maeneo au vijiji ambavyo vinapakana na hifadhi, habari za tembo kurudia njia walizopita miaka ya nyuma huwa ni nyingi. na hizi zote hutokana na uwezo wao wa kukumbuka nini walikipata walipopita zamani. Kama walipata neema, ni dhahiri hali ikiwa ovyo porini watarudi kupita tena hapo mahali.
kwa tembo, kiongozi wa kundi huwa ni tembo jike tena ambae mwenye umri mkubwa kushinda tembo wengine. Na huyu haingii madarakani kwa ubabe au mabavu, tembo wana utaratibu wa kupishana uongozi bila ya mikiki na mapambano. Kwa style hii, yule alnaeingia madarakani anakuwa ni mwenye uzoefu wa kutosha na kujua nini kinapatikana wapi kipindi gani. Hivi vyote vinachangiwa na kwa kuwa tembo huyo mzee anakuwa na kumbukumbu ya mengi aliyopambana nayo ktk maisha yake na hivyo anakuwa ktk nafasi nzuri ya kuepusha shari kwa kundi analoliongoza.
Advantage hii ya experience inakuwa haipo kwa wanyama ambao kiongozi anaingia madarakani baada ya mpambano. mara nyingi anayeingia madarakani huwa ni mdogo kiumri na anakuwa hajakutana na mengi ktk maisha yake ya kumfanya kuwa kiongozi bora. Kwa kifupi wengi huwa ni bora kiongozi. hali hii ipo kwa Simba, Viboko, Swala na wengi wengineo.
Tofauti yake inakuja kujionyesha kwa tembo ambapo daima hawaathiriki na njaa au ukame kwa kuwa kiongozi anauelewa wa wapi kwa kwenda ili kupata mahitaji.
Angalizo:Advantage hii ya experience inakuwa haipo kwa wanyama ambao kiongozi anaingia madarakani baada ya mpambano. mara nyingi anayeingia madarakani huwa ni mdogo kiumri na anakuwa hajakutana na mengi ktk maisha yake ya kumfanya kuwa kiongozi bora. Kwa kifupi wengi huwa ni bora kiongozi. hali hii ipo kwa Simba, Viboko, Swala na wengi wengineo.
Tofauti yake inakuja kujionyesha kwa tembo ambapo daima hawaathiriki na njaa au ukame kwa kuwa kiongozi anauelewa wa wapi kwa kwenda ili kupata mahitaji.
Picha zote ni Selous Game reserve; Ahsante ya picha TTB
Tusiuchukulie kwa juu-juu mtundiko huu na kuanza kuutafsiri sivyo ndivyo kwa maisha ya kazini ya binadamu
No comments:
Post a Comment