Tanzania yetu ni nchi kubwa sana, ukubwa wake unadhihirishwa na mambo mengi ikiwemo mgawanyiko wa hali ya hewa na maliasili. Kuna maeneo yanakuwa ktk baridi kali ilhali maeneo mengine yanakuwa kwenye joto kali na kwengineko mvua ikinyesha. ktk maeneo haya ndiko huko tunakutana na vivutio mbalimbali asilia ambavyo nchi yetu imejaliwa kuwa navyo. Mchanganyiko huu wa hali ya hewa na mazingira una mazuri yake na karaha zake kwa wewe unaependa kutembelea mbuga na hifadhi. Karaha utakayokumbana nayo ni kwamba unaweza kwenda sehemu na ukakuta hali ya mazingira ya mbuga au hifadhi haikuvutii. Hapa nikimaanisha mandhari na hali ya hewa. Uzuri wake ni kwamba kila mbuga utakayoitembelea itakuwa ni tofauti na nyingine kimandhari na hata hali ya hewa. Hii inakupa nafasi ya kuona kitu kipya unapoingia ktk mbuga au hifadhi nyingine.
Kikubwa ambacho naomba mdau ukielewe ni kwamba kila hifadhi iliyopo Tanzania ina muda wake mahususi wa kuitembelea ambapo vipengele vyote muhimu kwako vinakuwa vip ktk kiwango kizuri na bora; hapa nazungumzia hali ya hewa, mandhari na hata uwepo wa wanyama utakaopenda kuwaona ukiwa huko. Picha juu ni Sehemu ya mto unaomwaga maji ktk mto Ruaha, ndani ya hifadhi ya taifa ya Ruaha NP. kipindi cha kiangazi baadhi ya mito hukauka na kupotea kabisa kama ilivyo hapo juu.

Hali ya maji ikiwa mbaya, hata wanyama huwa wanapatika kwa shida sana mbugani. Kuna baadhi ya wanyama huhama maeneo kabisa kwenda kutafuta maji na malisho mbali na hifadhi au maeneo yanayofikika kirahisi. Mfano dhahiri wa hii dhana ni ile migration ya nyumbu na pundamilia kule Serengeti. Picha juu ni Tembo akiwa na mwanae kwenye moja ya mito iliyokauka ndani ya Ruaha National Park.
Picha juu inakupa hali halisi ya wapi maji hufikia wakati wa mvua (angalia kingo za huo mto) na wakati picha hii inapigwa (kiangazi) maji yako wapi. Hii yote ni ndani ya Hifadhi ya Ruaha
Ni dhahiri ya kwamba picha ya juu na hizi ambazo zinafuata hapa pichi zinakuvutia na kukuhamasisha zaidi kushinda zile za awali. Hizi picha zilipigwa kipindi baada ya mvua na kufanya ardhi kuwa na nyasi za kutosha kutoa hiyo green unayoiona na kustawisha afya za wanyama.
Sharubu wamekuja kupokea wageni wao; Ruaha NP
Licha ya kwamba tovuti za TANAPA na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) zina maelezo mazuri ya muda upi ni mzuri kutembelea maeneo kadhaa, Ni vyema sana ukapata ushauri toka kwa wenye uzoefu (Makampuni au mtu binafsi) ili kujua ni muda gani mzuri wa kwenda kutembelea hifadhi fulani. Nasema hivi kutokana na ukweli wa kwamba hali ya hewa nayo inabadilika sana na hii inaweza kuchangia ubora wa safari yako. Licha ya kwamba picha hizi ni za hifadhi ya Ruaha, lakini hali kama hii hutokea pia ktk hifadhi nyingine na tofauti yake ipo wazi. La sivyo unaweza kwenda huko muda ambao usiofaa na kujikuta haujaridhishwa na mandhari au hata wingi wa wanyama uliotegemea kuwaona ktk safari. Hizi safari zinagharimu pesa na muda hivyo ni vyema mgeni upate ushauri mzuri ili kuifanya safari yako iwe bora. vipengele vingine vinabaki kuwa ni sehemu ya adventure.

JAMANI NAOMBA KUULIZA HIVI HAO SIMBA HAPO PICHA YA JUU WANAWEZA KUKUVAMIA UKISHUKA PALE KWENYE NDEGE KUINGIA PALE KWENYE MABANDA?
ReplyDelete