Thursday, May 6, 2010

Mavazi yake asilia yanatambulisha rika lake

Kwenye jamii ya kabila la Wamasai, vazi ambalo atakuwa kalivaa mwana jamii, linaelezea fika yeye yupo ktk kundi-rika lipi. Picha juu ni mavazi ya vijana wa kiume. Hapo kuna mmoja kaenda jando na wakati mwingine bado hajakutana na kisu cha ngariba. Hayo ni baadhi ya mambo mengi ambayo unaweza kujifunza ukitembelea kituo cha mila na desturi ya wamasai kilichopo ndani ya Mesarani Snake park Arusha, nje kidogo ya jiji la Arusha (njia ya kuelekea Monduli).

Hapa ni mavazi ya akina dada na akina mama.

ukiachia fashion show ya mavazi ya wamasai, pia kuna picha zikionyesha shughuli mbali mbali za jamii ya wamasai. Hizo sanamu zinaonyesha mandhari na shughuli ya jando kwa wanaume. Ni dhahiri kabisa huyu kijana atarudi nyumbani akiwa na vazi tofauti na lile alilovaa wakati anapelekwa jando.

No comments:

Post a Comment