Monday, May 24, 2010

wahamiaji wa Serengeti

Kama hifadhi ya Taifa ya Serengeti ingekuwa ni nyumba, basi hawa jamaa wangestahili kuitwa wapangaji.
Hili lilikuwa ni kundi dogo tu la Nyumbu ambalo lilikuwa likihama toka Kaskazini kuja Kusini ambako ndio huwa mwisho wa mzunguko wao.

Walikuwa wametanda pande zote mbili za barabara wakisubiri tupite ili nao waendelee na safari yao.

Sijui niseme ni uwoga au umakini; kukitokea tofauti ndogo ktk mapito yao basi sharti wasimame na kuangalia hali ipoje na kisha waone nini cha kufanya.
Kuna dondoo moja nilipewa nilipokuwa Serengeti mwaka jana ni kwamba endapo nyumbu wa kwanza atavuka mbele ya gari lako. Basi nyumbu walio nyuma yake nao watataka wapite mbele ya gari lako na sio nyuma hata kama gari limesimama. Tena hali huwa mbaya zaidi kama utakutana nao usiku ukiwa umewasha taa za gari yako. Wote watataka wapite mbele ya gari yako (kwenye taa). watafanya hivyo hata kwa kulikimbiza gari lako sambamba hadi hapo utakapochochea zaidi. Na hata ukimpita, atasimama atafakari nini cha kufanya.

1 comment:

  1. ha ha ha ha, kweli Nyumbu ndivyo walivyo, huwa wanashangaa sana kama vile akili zao zimewapotea ghafla au zimepungua wanasubiri zijae ndipo wawaze. Nimecheka sana hawa wapangaji hawatulii, kazi wenda na kurudi tu.

    ReplyDelete