Wednesday, May 5, 2010

Twiga

Twiga ni mnyama wa porini ambae anaelezwe ya kuwa ndie mamalia mwenye blood pressure ya juu kushinda mamalia wote. blood pressure ya twiga ni mara mbili ya blood pressure ya Binadamu. Kinachosababisha hii hali ni ukweli wa kwamba moyo wake inabidi usukume damu kwa nguvu ili iweze kupambana na gravity ili kuweza kufikisha damu ktk ubungo wa twiga kwa wakati unaostahili. Hapo inamaanisha safari ya damu kwenda kwenye ubongo wa twiga inahitaji pressure kubwa. Kutokana na hali hii, inaelezwa pia miguu ya twiga ndio inapambana na pressure hii kwa sana. Licha ya shingo yake kuwa ndefu, lakini bado ipo ktk mfumo sawa na mfumo wa mamalia wengine wenye shingo - idadi ya pingili. Mamalia huwa na shingo inayotengenezwa kwa pingili 5; twiga licha ya urefu wa shingo yake, imetengenezwa kwa pingili 5 pia kama ya binadamu.

Jambo jingine ambalo linaweza kukuacha mdomo wazi kuhusu twiga ni kwamba hakuna ushahidi wa kama twiga anatoa sauti au la. Japo swala hili wanasayansi bado wanaendelea kulifanyia homework kila kukicha. Wakimfanyia upasuaji wanamkuta twiga ana viungo vyote vinavyohitajika kutoa sauti lakini hakuna ushahidi wa twiga akitoa sauti ya namna yoyote ile zaidi ya kishindo chake akikimbia. Hili ni jambo ambalo linawaumiza kichwa wanasayansi wa wanyama pori. picha juu ni twiga akila matawi ya juu ndani ya hifadhi ya Ruaha national park

3 comments:

  1. Hiyo ya sauti imeniacha mdomo wazi ki ukweli.
    Big up mdau kwa kutuelimisha kuhusu mambo ya hifadhi zetu. Tembeatz inanielimisha sana kuhusu mambo ya porini. Siku nikiingia porini, nadhani uelewa wangu utakuwa uko juu kushinda nilivyokuwa miezi 3 iliyopita.

    hivi twiga hana jina la porini kama Sharubu, wa chini au wa juu???

    ReplyDelete
  2. Anaitwa 'Matawi ya juu'

    ReplyDelete
  3. Mimi nilishawahi kutembelea baadhi ya mbuga nilisikia wakitaja MREFU au wakati mwingine MREMBO.

    ReplyDelete