Thursday, May 6, 2010

Bachelors herd

Ktk Jamii ya swala, dume moja ndio huwa kiongozi wa kundi la swala. Dume huyu huingia ktk utawala baada ya kumpindua dume aliyemkuta akitawala kundi husika. Kazi kubwa ya dume huwa ni kuzaa na majike kwa lengo la kuzaa na kulilinda kundi hilo. Kundi hili huundwa na maswala jike na madume wadogo.
Swala madume wadogo wanapoanza kukua na kuanza kutishia amani kwa dume kiongozi, Swala hao hutimuliwa kundi ili kupunguza shari kwa mtawala. Swala hao (waliotimuliwa) huunda kundi lao ambalo wataalamu huliita bachelors herd.
Kazi yao kubwa ni kujifua, kwa kupigana wenyewe kwa wenyewe mara kwa mara ili kuweza kuja kupambana na mtawala kwa lengo la kumpindua. Ikitokea mtawala amepinduliwa basi nae huja kuomba hifadhi ktk bachelors herd na kuanza routine za maozezi ili nae aje kumpindua atakae kuwa anatawala wakati huo. Kwa wanyama, jambo la uzazi linapewa kipaumbele na halina mzaha. mnyama akitaka kuendeleza uzao wake hupambana kwa namna yoyote ili ampate jike waanzishe familia yao, kwa wanyama hili humaanisha kupata mtoto. Issue ya malezi hapo habari hutofautiana kati ya jamii moja hadi nyingine.

Tofauti kati ya swala dume na swala jike ni uwepo wa pembe. Swala dume ndie mwenye pembe. Picha juu ni kundi la Swala waliokutwa na mdau ndani ya hifadhi ya Mikumi NP.

No comments:

Post a Comment