Wednesday, May 5, 2010

Sio bure... huu ulikuwa ni mtego; Serengeti NP

Nilipokuwa ktk pitapita ndani ya Serengeti NP, tuliwakuta hawa sharubu wawili wakiwa wamekaa ktk mkao ambao kiufundi, unaonekana ni mkao wa kazi - mawindo. Guide alituambia kuwa si bure, hawa jamaa hawajashiba na huo mkao ni ishara ya kuangalia ustaarabu mwingine unaendaje.
Licha ya kwamba Serengeti ni jangwa la nyasi lakini hawa Sharubu tuliwaona kama bahati. Inakuwa ngumu kuwaona hata wakiwa sehemu ya wazi kama walivyo hapo juu. Huu sio mkao wa mapumziko


Baada ya kuona tumeotea chezo, mmoja wao aliamua kuamka na kuanza kuangalia ustaarabu mwingine. Hapakuwa na wanyama wowote karibu na hili eneo ambapo tuliwakuta hawa sharubu. hii ilikuwa ni maeneo kusini mwa Hifadhi ya taifa ya Serengeti. Wote walikuwa ni sahrubu jike - ambao ndio wawindaji wakuu ktk jamii ya Sharubu.

2 comments:

  1. HEBU NIAMBIE MDA WOTE HUO MLIKUWA NDANI YA GARI?

    ReplyDelete
  2. Mdau,
    Picha zote hizo nimezipiga nikiwa kwenye gari.
    Ukiwa ktk hifadhi huruhusiwi kushuka toka kwenye gari isipokuwa ktk sehemu chache zilizoruhusiwa au hotelini.

    ReplyDelete