Wednesday, May 26, 2010

The Saddle, Mlima Kilimanjaro

The Saddle ni moja ya maeneo anapopita mpanda Mlima Kilimanjaro (Marangu route) wanapokuwa wanatoka Mawenzi kuelekea Kilele cha Kibo. Sehemu hii inachukua mandhari ya jangwa. Picha juu ni mdau (shoto) akiwa na msaidizi wake wakitafakari kabla ya kuendelea na safari na kuanza kukimega kipande cha the saddle. Kilele kinachoonoka kwa mbali (kilichofichwa na mawingu) ni Kibo, ndio huko mdau alikuwa akielekea.

Kibo ikionekana kwa mbali

Michirizi/mistari unayoiona ktk hicho kilima inatokana na upepo mkali unaokuwa unavuma sehemu hii.

Safari inaendelea

Ukifika mitaa ya kati unakutana na kibao kinachokueleza upo wapi.

1 comment:

  1. Mwisho wa umri wa mtu kupanda huo mlima ni miaka mingapi.

    ReplyDelete