Wednesday, May 26, 2010

Nje ya Ngorongoro crater kuna mambo pia...

Ukishaingia ndani ya NCAA baada ya kupita gate (ukiwa unatokea Arusha) na unaelekea kwenye lango la kushuka na kuingia crater, unaweza kupata bahati ya kuona baadhi ya wanyama ambao wapo nje ya Ngorongoro crater yenyewe (yaani lile shimo) lakini bado wamo ndani ya eneo la hifadhi. Sehemu hii unaweza kuwakuta wanyama wakubwa na wadogo kama uonavyp ktk picha ya juu. Tulidokezwa kuwa baadhi ya hao nyati ni resident - wanakuwa hapo muda mwingi.

Mateja nao wapo kwa sana, Uwepo wa miti nje ya Crater ndio unaowapelekea mateja kukaa muda mwingi nje ya Ngorongoro crater. Ndani ya crater miti sio mingi sana kama ilivyo nje ambapo inafunika sehemu kubwa ya eneo.

Hapo kulikuwa na Nyati pamoja na waterbuck.

Nyani aka mateja wakiwa wanahama toka upande mmoja wa barabara na kuelekea upande mwingine. Kundi lao lilikuwa na Mateja wa kutosha siku hii. Ngorongoro Crater yenyewe ipo upande wa kulia wa hiyo barabara.

Wakizidi kutokomea

No comments:

Post a Comment