Ukiwa unaenda Selous kwa barabara kupitia njia ya kilwa rodi, utafurahia lami mpaka Kibiti au Ikwiriri. Hizi ni sehemu mojawapo ambazo wageni wanaoenda selouos kwa barabara huchepuka na kuendelea na safari yao. Sehemu kubwa ya barabara hii ni ya vumbi lakini imeshindiliwa vyema.
Ni mwendo wa takriban saa moja na nusu hadi kufika Gate la Mtemere, safari ambayo itakupitisha ktk vijiji karibu 12 toka barabara kuu (kilwa Rodi) hadi utakapofika Kijiji cha mwisho (Mloka) kabla ya kuingia mbugani - Geti la Mtemere. Ukipata guide mweledi wa eneo hili, kuna mengi ambayo utaelezwa na kujifunza. Njiani utaona ushahidi wa ile amri ya kusitisha biashara ya magogo kwenda nje ya nchi. Utajionea magogo mengi yakiwa yametelekezwa pembezoni mwa barabara. Picha toka maktaba ya TembeaTz
No comments:
Post a Comment