Monday, May 3, 2010

mwayo wake, Ni timing tu....

Asikwambie mtu, kupiga picha wanyama wakiwa ktk mazingira yao asilia kuna hitaji timing na umakini wa hali ya juu. Nyakati nyingine bahati huchangia lakini si siku zote. hawa huwezi kuwaambia smile na ukategemea waka-smile ili utoe picha nzuri. Au uwaambie Banana... Mdau aliyepiga trip yake Selous aliweza kutumia vyema element ya timing na umakini na kunyakua taswira mwanana ya Sharubu na mwanae.

Mie ndio dah! bahati haikuwa yangu siku hii... hapo niliukosa mwayo wa huyu sharubu kwa tundu la sindano. Hii ilkuwa ni Selous pia, mwaka jana.

Documentary (ya dk 30) ya maisha ya mnyama au tabia fulani ya mnyama wa porini huchukua muda mrefu kuitengeneza. Ukweli ni kwamba muda mwingi unaishia kumfuatilia mnyama na mchache unakuwa ndio wa kupiga picha zenyewe. Ndio maana wanaotengeneza documentary za wanyama pori huishia kuishi porini kabisa au kwenye zoo kwani hutumia muda mwingi kufanya kazi ya muda mdogo.

No comments:

Post a Comment