Friday, May 28, 2010

Msaada kwenye tuta.... Migration ya Serengeti

Pole kwa Shuguli Kk, Ahsante sana kwa habari na elimu maarifa unayotoa kuhusu vivutio mbalimbali vya hapo Nyumbani. Unatusaidia kupata uelewa mzuri wa nchi yetu.
Mimi nina jambo moja na naomba msaada wako na kama itakuwa ngumu, si vibaya ukiliweka jambo hili ktk blog ya Tembea Tz nipate kujua toka kwa wadau wengine wenye kuweza kutoa jibu.


Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ni maarufu sana kwa lile tukio la Nyumbu zaidi ya milioni moja na ushee ambao huhama toka Serengeti kuelekea hifadhi moja iliyopo nchi jirani na kurudi tena Serengeti. Ni Tukio la kipekee sana na lina maelezo mengi ya kuvutia. Wengi huitembelea hifadhi yetu hii kuona tukio hili. Jambo moja ambalo linanitatiza ni kwamba; Licha ya Kwamba Nyumbu wanapatikana karibu ktk hifadhi na mapori yote hapo Nyumbani, lakini mbona sijawahi kusikia Nyumbu wa Mikumi wakihama toka Mikumi kwenda sehemu nyingine au humo humo ndani ya Mikumi? Ni kitu gani hasahasa kinachowafanya Nyumbu wa hifadhi nyingine wasiwe na Migration yao?


Nakutakia kazi njema,
Mdau 'Ukerewe'

1 comment:

  1. YAANI KWELI HATA MIMI HICHO KITU NILISHAWAHI KUJIFIKIRIA. MWENYEJI WETU ATUWEKEE MAJIBU PLZ

    ReplyDelete