Sunday, May 30, 2010

Mrefu ndani ya Lake Manyara

Twiga aka Mrefu akiwa anavinjari ktk moja ya maeneo yalio wazi ndani ya hifadhi ya Manyara. Kumbuka ya kwamba sehemu kubwa ya hifadhi ya taifa ya Manyara ni msitu. Hii sehemu ya wazi ipo pembezoni kabisa mwa ziwa Manyara lenyewe. Twiga huyu ni wa aina ijulikanayo kama Maasai; Maasai giraffe.
Kimsingi, kuna aina 3 za twiga; Maasai (ambao ndio wengi hapa nyumbani), Reticulated na wengine ni Rothschild. Hizi aina nyingine mbili zinapatakan kwa chati hapa kwetu. Tofauti yao ni mfumo wa hayo mabaka yao. Nimejaribu kupekua maktaba ya TembeaTz nimejikuta nina taswira za Maasai Giraffe peke yake.

No comments:

Post a Comment