Sunday, May 30, 2010

Ni Kilimanjaro Kempinski hotel, Dar


Awali niliwahi uliza wadau watueleze hii picha ilipigwa wapi au inaonyesha mandhari ya wapi. Wapo waliojaribu na kupatia, wapo pia waliokiri kuomba msaada kwa wadau zaidi na wapo walioingia chaka kabisa. Yote kwa yote, napenda kuwashukuru nyote mliojaribu kubashiria. natumai hata wale ambao hawakutuma ubashiri wao, mtundiko huu uliwapa changamoto kidogo.

Picha hii inaonyesha mandhari ya Bwawa la Kuogelea la hotel ya Kilimanjaro Kempinski Dar-Es-Salaam. Baada ya kufanyiwa ukarabati, Bwawa la kuogelea la hoteli hii lilihamishiwa ghorofani badala ya kule nyuma lilipokuwepo awali. Nadhani wadau wa disko la enzi hizo la pool side mnalikumbuka eneo lenu la matukio vyema! Enzi hizo hotel hii ikijulikana kama Kilimanjaro Hotel na kumbi yake maarufu ya mikutano iliyojulikana kama Simba Grill.
Mimi nalikumbuka sana lile bwawa la zamani la kuogelea kwani weekends (wakati nipo Shuleni) nilikuwa sikosekani hapo kupiga mbizi na wadau kadhaa tuliokuwa tukisoma wote. Ahsante ya picha-TTB.

No comments:

Post a Comment