![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgur38iV5CtVCswBmJtMWcS5LkZAy00gPGfr8VatcZurHKiHJsB3RiN5hKqE5hH8vRgUSiS7oTMI6nMDQvSF2b_nsFL9_vqLjcN62GC0LzU9F4NH1ca3f86pkdX4ZVuRxYkZcVHWFyuKTks/s400/01.jpg)
Matukio mengi ya watu kuuwawa na kisha kuliwa na wanyama wakali nje ya hifadhi huashiria kuwa mnyama aliyehusika na tukio hilo, ameishiwa nguvu za kupambana na wanyama wenzie na hivyo anatafuta chakula ambacho ni rahisi kwake kukipata - Binadamu.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhChrbVsTFmIf5GOgkq9be-zweIq5qIzXVXbGT-MN3H3_z4LFBpSJer98SgRqs03j8y5P6QkRD7In_VeX-WPS0h0s_fvLmlmHTEYzE2qf29_iZeCF0ZdmrFK_kFANhgJlXd4o7TfD4mDSr8/s400/02.jpg)
Unapokuwa unaenda Selous kwa gari, kupitia njia ya Kibiti au hata Ikwiriri, utapita kwenye moja ya vijiji (jina limenitoka) ambapo utakuta na hilo bango lenye kumbukumbu ya Simba aliyevamia eneo hilo akitokea hifadhi ya Selous na kuua watu 40 kabla na yeye kuuwawa tarehe 20-4-2004 kama inavyoelezwa kwenye bango.
Uchunguzi uliofanywa kwa Simba huyo baada ya kuuwawa ulibainisha ya kuwa alikuwa ni simba Dume mzee, aliyepoteza moja ya meno yake ya mbele ambayo ni muhimu sana ktk shuguli ya mawindo yake.
Simba huuwa mnyama kwa kumnyima hewa (Suffocation), hufanya hivi aidha kwa kuziba koo (wind pipe) au hata wakati mwingine kufunika pua ya windo lake na kumkosesha hewa kabisa. Simba anapoondokewa na moja meno yake ya mbele (Canine), huwa anakosa uwezo wa kung'ata na kumng'ang'ania mnyama anayemuwinda ili kumuua. ktk hali hii huanza kutafuta kitoweo ambacho ni rahisi kukikamata na anapomuua mwanajamii na kugundua kuwa ni rahisi zaidi kushinda kumkamata nyumbu au swala, Simba huyo ni lazima atarudi tena kuja kumkamata mwanajamii mwingine. picha zote ni toka ktk maktaba ya tembeaTz;
Tukio likitokea ndani ya national park inakuaje? Simba atauwawa pia au ataachwa huru kwakuwa yupo ktk eneo lake la kujidai kama golikipa?
ReplyDeleteMdau