Siku chache zilizopita nikiwa ktk hatua za mwisho kujianda kuelekea nyumbani, nilipata barua pepe toka kwa Da' Subi ambayo aliituma kupitia (tembeatz@gmail.com) ili kupata mawili-matatu kuhusu swala zima la Utalii wa ndani. Ilinilazimu nisitishe mchakato wa kuondoka ofisni ili niweze kutoa maelezo ambayo ningeweza kumpa kwa taarifa alizokuwa kanipatia. Email yake ilikuwa kama ifuatavyo;
Salam mhusika wa Tembea Tanzania,
Mimi ni mmoja wa watu wanaotembelea tovuti yako kila mara na kupokea picha na taarifa kupitia RSS feed. Asante kwa kutupa picha za kuonesha madhari
tofauti tofauti zilizomo katika nchi yetu.
Nina swali ambalo najua hapa ni mahali muafaka pa kupata majibu yanayoridhisha.
tofauti tofauti zilizomo katika nchi yetu.
Nina swali ambalo najua hapa ni mahali muafaka pa kupata majibu yanayoridhisha.
- Je, mtalii wa ndani (mzawa) akitaka kutembelea mbuga, ni mbuga gani ni rahisi kufikika na kutembelewa katika kipindi cha mwezi Juni?
- Je, njia rahisi ya kufika katika mbuga yoyote ni kwa kutumia kampuni ya utalii au kukodi gari na kujiendea binafsi?
- Je, ni hoteli au nyumba gani za wageni zenye bei nafuu kwa Mtanzania wa kawaida kufikia uwapo nchini Zanzibar?
Asante!
Naomba ushauri wako tafadhali na mwongozo katika kupanga safari ya utalii wa ndani.
Subi|www.wavuti.com
bofya hapa upate kujua TembeaTZ ilitoa ufafanuzi gani kwa Da' Subi kutokana na maswali yake. Lakini pia TembeaTz inakupa nafasi nawe kuchangia ktk hili kwa kutoa maoni yako kwa kutumia sehemu ya maoni ktk mtundiko huu. Karibu sana
WOW!!!
ReplyDeleteKK. Sina ninaloweza kusema zaidi ya kukushukuru na kukutakia kila lililo jema. Nimetembelea leo na NIMEJIFUNZA MEEENGI SAANA.
Ntaiweka blog hii kwa WADAU wengine waione a kujifunza pia. Hasa kwa sisi tulio nje ambao wakati mwingine maswali haya huwa hatuna majibu yake.
Blessings