Monday, May 3, 2010

Kituo cha taarifa, Serengeti

Ndani ya hifadhi ya Serengeti kuna kituo ambacho mgeni anaweza kwenda na kupewa taarifa mbalimbali za hifadhi na vile vinavyohifadhiwa ndani ya hifadhi hii pekee ya Serengeti. Kituo hiki kipo kati kati ya Serengeti, eneo lijulikanalo kama Seronera. Hapa utapata historia ya eneo, matukio muhimu yaliyotokea na jinsi yanavyotokea ktk kipindi cha mwaka. Kwa bahati mbaya siku hii tulipita hapa mida ya jioni na hoteli tuliyofikia ilikuwa ni wendo kidogo toka hapa, hivyo hatukuweza kuzunguka ndani ya kituo na kupata taswira. Hii inatokana na sheria ya kwamba hakuna mgeni anayeruhusiwa kufanya safari ndani ya hifadhi ifikapo saa 12jioni.

No comments:

Post a Comment