Monday, May 3, 2010

Campsite namba 1, Arusha National Park

Hili eneo ni eneo maalum ndani ya Hifadhi ya taifa ya Arusha national park kwa ajili ya camping. eneo ni kubwa na la kutosha na limezungukwa na miti ambayo imetawala sehemu kubwa ya hifadhi ya Arusha. nyumba nyeupe unayoiona ni kwa ajili ya huduma binafsi. maeneo ya kufanya camp hutofautiana kutokana na uoto na mazingira ya mbuga husika. lakini kila unapoingia kwa ajili ya kufanya camping, lazima utapewa guide mwenye Silaha wa kukulinda kipindi chote utakachokuwa porini. malipo haya unayafanyia gateni ubnapokiwa unaingia. mgeni inabidi uje na nondo zako za camping, kuanzia vifaa vya kulalia na hata vya kukuhudumia kwenye maankuli.

Ushauri wa bure kama unataka ku-enjoy camoing ni vyema utafute mtaalam (au kampuni) inayojishughulisha na camping na uichie iandae safari - hasa hasa mkiwa kundi kubwa la wadau. Mdau JSK toka Moshi aliweka kambi siku si nyingi ktk eneo hili na turushia taswira hii mwanana.

1 comment:

  1. Angalau leo nimepata mwanga wa campsite inakuwa na mazingira ya namna gani. Ipo siku nitafanya camping porini.

    ReplyDelete