Wednesday, April 28, 2010

Ngurumo za Sharubu

Ieleweke ya kwamba ni sharubu dume pekee ndiye anayeunguruma porini. Dume huunguruma ili kuwapiga mkwara madume wengine wasizengee majike yake na kamwe wasithubutu kuingia kwenye himaya yake. ktk mazingira haya, ngurumo hutumika kama njia ya kutoa warning kwa wavamizi na wadoezi pia.

kuna jambo moja ambalo nimewahi kulisikia na kwa bahati mbaya sijabahatika kupata ushahidi wake. Hili swala linahusiana na usikivu wa ngurumo za sharubu.
Niliwahi kusikia kuwa endapo ukisikia sharubu anaunguruma na sauti ya muungurumo wake ikashiria kuwa yu mbali na ulipo, basi ujue huyo sharubu yupo karibu sana nawe. Dhana hiyo inaenda mbele na kusema kuwa unaposikia kuwa muungurumo ni mkali (sauti ya juu), basi ujue sharubu anayeunguruma yu mbali nawe.
Kwa bahati mbaya sana sijawahi kuwa porini na kumshuhudia sharubu akiunguruma mimi nikiwa karibu nae na kukisia intesity ya mlio wake na kujua ukweli. Mara ya mwisho kusikia ngurumo za sharubu ilikuwa ni mwaka jana nikiwa Serengeti lakini sikuweza kuthibitisha chochote kwani ilikuwa ni usiku na sikuwa na jeuri ya kutoka nje na kuanza kutafuta ukweli.

Naomba tusaidiane wadau ktk hili, kuna ukweli wowote au ndio porojo za vijiweni?

3 comments:

  1. HALOO KWELI WADAU WATUSAIDIE HATA MIMI KITENDAWILI HICHO SIJAWA KUKITEGUA

    ReplyDelete
  2. Wadau, mimi nimekuwa na experience ya hiyo mingurumo ya simba mara kadhaa. Mara nyingi tukianza kusikia wenyeji huniambia yuko kama kilomita tatu halafu baadae hunieleza sasa yuko kilomita mbili ambapo mngurumo huongezeka na mwishowe unasikia kwa nguvu zaidi, wakati huo anakuwa amefika kama nusu kilomita. Mara nyingi anakuwa ni dume aliyepoteza pride yake kwa dume kijana so anakuwa anahangaika kwa ajili yuko embarassed, na ndiyo maana huwa anatembea haraka

    ReplyDelete
  3. Kaka fanya safari, maana ni muda kila nikifungua namkuta masharubu tu, Pita hata mitaa yetu tuuone Uhuru wetu na barabara yetu.

    ReplyDelete