Tukiwa tunaendelea kukuhabarisha kuhusu kipengele cha muda muafaka wa kwenda na kutembelea mbuga mbalimbali hapa Tanzania, safari nakuletea taswira toka hifadhi ya taifa ya mikumi zikikuonyesha hali halisi ilivyo ktk vipindi viwili tofauti; Kipindi cha kiangazi na kipindi baada ya mvua.
Chini ya huo mti kulikuwa na sharubu wanapumzika. Kamera ya mdau ilikumbana na changamoto alipojaribu kuwavuta karibu ili waonekane vyema.
Wa Juu (Chui) akiwa anavinjari pembezoni kabisa mwa ile hippo Pool ya Mikumi. Wengi waliotembelea hifadhi ya mikumi wanaifahamu hii hippo Pool. Sehemu hii ni moja ya sehemu ambayo wageni wanaruhusiwa kushuka toka kwenye gari na kujinyoosha/kutembea. Picha juu ni ishara ya kwamba usishuke kichwachwa na kamwe usicheze mbali na gari yako. Jamaa huja karibu kufanya patrol
Sharubu jike. nakumbuka hii picha iliwahi kuzua mgogoro kuhusu simba jike naye kuitwa sharubu. Wengi walitegemea kuwa jina la Sharubu hutumika kwa dume pekee.
Picha zifuatazo na kuendelea (chini) ni picha ambazo mdau Thom wa Kimasafaris alizipiga alipokuwa Mikumi mwaka jana. Ni Picha ambazo tofauti yake na picha zilizotangulia ni kwamba hizi zilipigwa kipindi cha ukame. Nadhani tofauti ipo wazi kabisa. Picha juu ni gate kuu la kuingilia ktk hifadhi. Geti hili lipo eneo linalojulikana kama Kikoboga. makao makuu ya hifadhi yapo eno hilo hilo, karibu kabisa na geti hili.
Swala hupenda kuzengea chini ya miti ambako huwa wanakutana na mabaki yanayodondoshwa na ngedere wanapokula matunda ya mtini. Maganda na mabaki wanayodondosha ngedere/nyani ndio huwapa lishe swala hawa.
Nia na madhumu ya mitundiko hii (kila hifadhi ina muda wake...) ni kujaribu kukupa hali halisi itakayofanya mdau kufanya safari yako muda muafaka ya kwenda ktk hifadhi. Njia rahisi ya kujua jambo ni kuuliza kwani wahenga walisema mwanzo wa werevu ni kuuliza.....
Unaweza kutembelea tovuti ya TANAPA au Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) ambako kuna dondoo zaidi kuhusu muda mzuri wa kutembelea mbuga na sehemu nyinginezo zilizopo ndani ya nchi yetu.
Mtundiko huu umeundwa kwa picha toka kwa Mdau ANM, Thom wa kimsafaris na baadhi toka ktk maktaba ya TembeaTz.
Unaweza kutembelea tovuti ya TANAPA au Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) ambako kuna dondoo zaidi kuhusu muda mzuri wa kutembelea mbuga na sehemu nyinginezo zilizopo ndani ya nchi yetu.
No comments:
Post a Comment