Mara nyingi ninapokuwa porini, huwa napenda kuianza siku mapema sana. Kawaida saa moja kamili unikuta niko mbali na eneo nililolala (kama nililala ktk hotel au lodge iliyopo ndani ya hifadhi) au nipo gateni nikikamilisha utaratibu wa kuingia ktk hifadhi na kuendelea na mizunguko. Siku moja (mwaka jana) ratiba ilikuwa tofauti kidogo ambapo ratiba ilikuwa ni kupumzika siku hiyo baada ya game drives za takriban siku 4 mfululizo. Ilipofika mida ya asubuhi, nilishtushwa na mlio wa kitu kikigonga kwenye kioo cha dirisha la balcony ya chumba nilicholala.
Alikuwa ni ndege aitwaye Hondohondo. walikuwa wawili na mmoja alikuwa amesimama kwenye hicho kiti na alikuwa akijarabu kubishana na kivuli chake kwenye kioo cha mlango. nilipoamka kuifuata kamera yangu, akaruka na kwenda kukaa hapo anapoonekana ktk picha za juu. Its a trully natural wake up call maana baada ya hapo sikuendelea kulala zaidi. hizi ni baadhi ya surprise ambazo unaweza kuzipata ukiwa porini.
Sababu inayonifanya nipende kuanza mizunguko asubuhi ni kwamba mida hii ni mida ambayo sehemu kubwa ya wanyama ndio wanakuwa wanaamka na kuanza kujipanga kwa siku yao mpya. na pia hata kwa wale ambao shughuli zao nimida ya usiku nao wanakuwa wanajipanga kutafuta sehemu ya kulikwepea jua. Maana huwa hawezi kujua kama kivuli atakachokichagua kitamfaa mpaka pale jua linapokuwa limechomoza kiaina. Ki Ukweli muda wa asubuhi una raha yake kwa game drive kwa mgeni. by the time jua limekuwa kali mnatufata mahali pa kupumzika na kumalizia siku kwani mnakuwa mmeona vya kutosha kama timing yenu ilikuwa ni nzuri
No comments:
Post a Comment