Monday, May 17, 2010

Empakaai Crater

Tanzania kuna Crater nyingi; hii hapa inaitwa Empakaai; Ni mojwapo ya maeneo mwanana ya utalii yanayopatikana ktk ukanda wa kaskazini wa utaliii. Mlima unaonekana kwa mbali kulia ni Oldonyo Lengai.
Wageni wanaoitembelea Empakaai Crater huwa wanaingia ktk crater kwa miguu (bila ya usafiri wa gari). Safari ya kushuka na kuingia ndani ya crater inaweza kuchukua takriban dakika 30. Mizigo hubebwa na punda.
Eneo hili lina ndege wengi wenye rangi na nyimbo nzuri za kukuvutia. Wanyama wanaopatika ndani ya crater ni wanyamaa jamii ya swala, Ndegere, Nyati (japo sio wengi sana) na wanyama wengineo ambao sio wala nyama. Sambamba na wanyama ndani ya crater kuna mimea na maua mengi ambayo huvutia pia.

Sehemu kubwa ya crater imezungukwa na ziwa ambalo maji yake ni alkaline. Flamingo wapo kwa sana ktk hilo ziwa. Ahsante ya picha, Antelope Safaris.

No comments:

Post a Comment