Monday, May 17, 2010

Matunda ya porini; Arusha National Park

Hifadhi na mapori ya tanzania hayaishii kuhifadhi wanyama peke yake, kuna mimea na matunda kedekede ambayo nayo ni sehemu ya mapori na hifadhi hizi. Mdau JSK alipotembelea Arusha national park na kufanya game walking safari alipata fursa ya kujionea matunda mbali mbali yanayopatikana ndani ya hifadhi hii. Picha juu ni matunda ambayo wenyeji wanayaita matunda ya nyani. hii inatokana na ukweli kwamba Nyani ndio wanaongoza kwa kuyala matunda haya.

Hizi ni strawberry ambazo kwa kuwa zimeshamiri porini, wenyeji wanaziita strawberry mwitu/pori.

Strawberry mwitu kwa karibu zaidi. Strawberry kwa kiswahili zinaitwaje?

3 comments:

  1. Haluu!!, Umenikumbusha mbali mtu wangu. Haya matunda tulikuwa tunakula tulipokuwa tunaendaga kuokota kuni za shule kwenye ule msitu chini ya mlima Kilimanjaro pale Rombo Mkuu (Mokala).

    ReplyDelete
  2. Haya matunda yanaitwa Nkerere !

    ReplyDelete
  3. hizo ni Rasberry au Rasberies kwa wingi. strawberries ni tofauti.

    ReplyDelete