Joto la mwili likipanda kupita kiwango kinachostahili, huweza kupelekea baadhi ya viungo vya mwili wa kiumbe hai kuanza kushindwa kufanya kazi au kupoteza uwezo wake moja kwa moja. Hili lipo kwa wanyama pori pia. Inapotokea kuwa joto la mwili linapanda kuzidi kiwango cha kawaida, ni lazima mnyama atafute namna ya kulishusha lifikie ktk kiwango kinachohitajika. picha juu ni mbuni ambao mdau Tom wa Kima safaris alikutana nao ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Tarangire wakipambana na hali hii kwa kutanua na kushusha mabawa yao. Hii inaruhusu hewa kupenya na kupunguza joto la mwili na kumweka mnyama ktk hali ya joto inayostahili.
No comments:
Post a Comment