Mkasi (mamba) huyaacha maji na kuja nchi kavu kwa sababu kuu mbili, Kuota jua au kuja kutaga na kulinda mayai. Mamba huyu alikutwa na wadau pembezoni mwa mto Rufiji ndani ya pori la akiba la Selous akiwa anarudi majini baada ya kuota jua vya kutosha. Mamba anahitaji kuota jua ili aweze kurekebisha joto lake la mwili. Licha ya ukubwa kiumbo, Mambo ni mnyama mwenye damu baridi. Anahitaji joto toka ktk chanzo kingine ili kimsaidie kuweza kunyanyua hali ya joto la mwili wake.
Wakati mwingine mkasi huonekana kama anakuwa anasotea tumbo anapokuwa anatembea, lakini ukweli ni kwamba anao uwezo kuunyanyua mwili wake wote toka ardhini na kutia mbio ikibidi. Hapa alikuwa hana pressure kwa hiyo alikuwa anatembea kwa maringo na madaha.
No comments:
Post a Comment