Wednesday, May 26, 2010

The Saddle, Mlima Kilimanjaro (2)

Mnapo panda mlima Kilimanjaro, chakula mtakachokula wakati wa mchakato wa kupanda mlima mnakuwa nacho. Kinakuwa kimebebwa na porters. Mida ya maakuli ikiwakuta mkiwa njiani, basi kuna sehemu nyingi maalum ambazo zimetengwa mahususi kwa ajili ya kupata msosi. Picha juu ni moja ya picnic site ambayo ipo ndani ya eneo la Saddle. Mkifika hapo kikosi kazi mlichoambatana nacho kitafanya mambo yote kufanikisha zoezi zima la maakuli.



Unapokuwa unaupanda mlima unakuwa unapata fursa ya kukutana na majira na mazingira mbalimbali ambayo mengine unaweza ukasema kama vile unaangalia Video ya NASA inakuonyesha ardhi ya Mwezini.
Ukiwa njiani utapita ktk maeneo ambayo ni misitu minene, kuna sehemu za majangwa kama saddle, kuna sehemu kuna uwanda wa nyasi fupi unaofanana na hifadhi ya Serengeti. Zipo crater kadhaa ambazo zinafanana na Ngorongoro crater kimaumbile na mwisho kabisa unakutana na Barafu (kibo, Uhuru peak). Ki ukweli Mlima kilimanjaro ni mkusanyiko wa hali ya hewa na uoto asilia ambao unaweza kumfanya mtu asielewe yupo wapi. Kila ngwe ktk safari ina mandhari yake na mvuto wake wa kipekee. Huu ndio mlima Kilimanjaro uliopo Tanzania pekee.

No comments:

Post a Comment