Ni Mti unaitwa Mkongo. Mbao zake ni maarufu sana kwa wajenzi. Ni aina ya zile mbao zijulikanazo kama mbao ngumu - hardwood. Unapatikana kanda za kusini na hata huko mikoa ya kanda ya kati.
Hii ni moja ya faida ya walking safaris, unapata fursa ya kusogelea vitu vingine ambavyo huku mjini unaviona vikiwa ktk hali tofauti. Mbao za mkongo nimeziona mara nyingi sana ktk sehemu zinazouzwa mbao, lakini mti unaotoa mkongo nilikuwa sijawahi kuuona. Hii ilikuwa ni mara ya kwanza (Sept 2008). Picha ilipigwa ndani ya pori la akiba la Selous game reserve. Mbao za mkongo zinachuana na mbao za mti mwingine ujulikanao kama mninga.
No comments:
Post a Comment