Wednesday, April 21, 2010

Kumbukumbu ya mvua za El-Nino za mwaka 1998

Kutembea kwingi ni kuona mengi; Kwa kawaida tumezoea kuona na kusikia kuwa mimea huhitaji maji ili iweze kuota na kukua vizuri. Ndio maana hata mvua zinapochelewa kunyesha ktk nchi zinazotegemea mvua kwenye kilimo, tawala huanza kuhaha kutafuta namna ya kulinusuru taifa ktk baa la njaa kutokana na ukame. Hali niliyoikuta Selous ilikuwa ni tofauti kidogo na mpaka sasa ukienda huko, utakutana na hali hii. Kama unavyoona ktk mtundiko huu, kuna kitendawili ambacho kinaweza kukuweka njia panda. Selous, kuna baadhi ya mimea ambayo hufa endapo itapata maji mengi kupita kiasi. Kipindi cha mvua, kina cha maji huongezeka na kuvuka mipaka ya kawaida.

ktk hali hii, maeneo ambayo yanakuwa nchi kavu wakati wa kiangazi, huzama na kuwa sehemu ya mto. Mimea iliyoota ktk maeneo haya nayo inajikuta ikupotea au kuzungukwa na maji kila upande. Ipo baadhi ya mimea ambayo itastahimili wingi huo wa maji na kuendela kuishi na ipo ambayo itaangamia kutokana na kupata maji zaidi ya kiwango chake cha kawaida. picha mbili za juu ni ushahidi wa mimea ambayo huangamia kwa kupata maji mengi. Inaelezwa kuwa miti mingi iliangamia kipindi cha mvua za El-nino za mwaka 1998 ambapo kina cha maji kilipitiliza na kudumu ktk level ya juu kwa muda mrefu tofauti na inavyokuwa kawaida. Baadhi ya miti bado inasimama mpaka leo licha ya kwamba imeshadhurika. Mingine ilianguka na kuoza.

Hii ndio ile miti ambayo inastahimili na kuendelea kudunda licha ya kuzungukwa na maji kila kona. Pichani ni Palm tree ambayo imeota ndani ya moja ya Ox-Bow lake mojawapo lilipo ktk mto Rufiji ndani ya pori la akiba la Selous Game reserve. Miti ambayo inadumu mpaka sasa inakupa picha ya level ya maji ilipofikia kipindi cha El-Nino.

Ni dhahiri kabisa juhudi za uhufadhi wa hili pori haziishii ktk kuhifadhi wanyama pori na mazingira peke yake, bali hata matukio muhimu ya hali ya hewa yanayoikumba dunia yetu yana kumbukumbu zake ndani ya hili pori. Hii leo huku mijini sidhani kama kuna kumbukumbu yoyote itakayoweza kutukumbusha purukushani za mvua ambazo zilileta maafa makubwa ktk sehemu zilizonyesha hapa nchini na duniani kwa ujumla. Ni Takriban miaka 12 imepita lakini bado pori la Akiba la selous linatunza na kuhifadhi kumbukumbu za tukio hili. Miti hii (iliyosimama licha ya kuangamia) ingekuwa ktk maeneo ambayo sio hifadhi ni dhahiri ingekuwa imeshageuzwa kuni siku nyingi mno.

Wadau, hivi Palm tree kwa kimatumbi unaitwaje?

No comments:

Post a Comment