Tuesday, April 20, 2010

La Gemma Del Est Beach Hotel; Nungwi Zanzibar

La Gemma Del Est ni moja ya hoteli kubwa ilivyopo visiwani Zanzibar ktk kisiwa cha Unguja. Hotel hii ipo kaskazini kabisa mwa Unguja, eneo lijulikanalo kama Nungwi. Picha juu ni moja ya Bar za hotel hii ambayo imejengwa juu ya maji.

Upande huu ni Bwawa la kuogelea na sehemu ya pwani ambayo mgeni anaweza kupumzika. Wageni wanaotembelea visiwa vya Zenj huja kwa ajili ya kulifuata jua na kupumzisha akili wakiwa ufukweni mwa bahari. La Gemma ina sehemu murua kwa wageni wenye mahitaji haya.

Curio shop ipo pia

Mandhari ya chumbani


La Gemma inavyoonekana tokea baharini. Vyumba vya hotel ni hivyo vioo unavyoviona ktk huo mteremko. Hotel hii imejengwa ktk cliff. picha hii niliipiga nikiwa katika Jahazi. Jikumbushe mtunduko kuhusu safari za Majahazi ya Zanzibar kwa ku-bofya hapa

Kijua kikizama huku mdau akipiga zake makasia ktk conoe yake. Ki matumbi cha canoe nadhani kitakuwa ni mtumbwi tu, maana hivina tofauti kubwa kimuonekano.

Bofya hapa kwa dondoo zaidi kuhusu hii hotel
-----------
Wadau samahi kwa ucheleweshwaji wa mitundiko, jana blog ilipata changamoto za kiufundi ktk kupandisha picha. leo mambo mswano, tunaendeleza libeneke.

2 comments:

  1. HIVI UNAJUA UKIWA NA MIMAWE HAMNA HAJA YA KUKIMBILIA ULAYA, MIRAHA YOOOTE UNAIFANYIA HAPAHAPA

    ReplyDelete