Tuesday, April 27, 2010

Usiku wa porini una mengi mengineyo..

Siku moja mwaka 2008 nilikuwemo ktk kundi kubwa la wazalendo ambao walijikusanya na kwenda kutembelea pori la akiba la selous. Tulipangwa kufikia Ndovu camp. Kutokana na wingi wa idadi ya wageni, ilibidi camp ifanye mpango wa kupeleka baadhi ya wageni ktk kambi nyingine iliyo karibu na hapa. Ktk mchakato wa kuamua nani alale wapi na nani, likaibuka kundi la watu 4 (mimi nikiwa mmoja wao) ambalo liliamua kulala sehemu ya juu kabisa ya hilo jengo - hapo kwenye viti na makopo ya maua yakining'inia. Tuligoma katukatu kwenda kwenye hiyo kambi kwa sababu tuliona ipo mbali kidogo na mpaka wa pori, hivyo tulihisi tungekuwa kama tunarudishwa mjini vile. japo baadhi yetu tulikubaliana na hili shauri kwa shingo upande - kipindi kile. Giza lilipoanza kuingi na muda wa kwenda kulala ulipotimu ndio hapo kiuoga kilipoanza kusogea, kilichokuwa kinatupa jeuri ni kwamba ktk ghorofa ya kwanza ya hilo jengo kulikuwa na chumba ambacho ndicho tulistahili kulala. lakini kwa kuwa tulikuwa tunataka kuwa karibu na nature ndio tukaenda kulala juu. Plan B tuliyoiweka ili kujipa moyo ilikuwa ni kuhakikisha kuwa chumba cha mlango ule haufungwa usiku ule ili kama kuna shida yoyote tukimbilie ndani.

Godoro unaloliona juu, ndio mimi na jamaa mwingine tuliegesha hapo huku wengine wawili walegesha kwenye viti 'makochi' unayoyaona pembeni. Licha ya kwamba tulichoka kutokana na safari ya takriban masaa 3 ya kutoka Dar , lakini usiku kuna nyakati tulikuwa tunashtushwa na kelele za wanyama na ndege. Usiku ule tulisikia milio ya ndege wengi mno wa porini wakiimba nyimbo zao. Camp haipo mbali na mto rufiji, hivyo tambo za viboko dume nazo tulizisikia usiku kucha. Ilipokaribia kuchwa, bwana afya (fisi) nae alipita karibu kabisa na kambi na akatoa mlio ambao ulituamsha wengi. Aliendelea na hamsini zake na kutuacha sie viroho vikidunda na kijasho chembamba kikitutoka. Tembo nao tuliwasikia kwa sana wakitoa milio yao, japo wao walisikika kwa mbali kidogo lakini tuliwasikia. Usiku huu hawakusogea kambini kabisa kwani ni jambo la kawaida kwa wao kuja hapa kambini mida ya usiku au jioni kabla jua halijazama.

Usiku huu ndio nadhani ulionitoa uwoga wangu wote kuhusu mambo ya porini. Mwanzo nilipatwa na woga lakini siku iliyofuata, idadi ya watu tuliokuja kulala nje ktk huu mjengo iliongezeka baada ya mdau mmoja aliyeenda kulala ktk camp mbali na hapa kuhamasika na simulizi za usiku. picha ni sehemu tuliyolala ikionekana baada ya jua kuanza kuangaza.

Hii picha niliipiga jioni wakati nikiangali options za mahali pa kulala. Kwa wakati ule, sikuwa na imani na kulala ktk hema dogo kama hili nililokuwamo ndani. Na kilichonitisha zaidi ni maelekezo ya kwamba nikilala humu ni lazima niingize viatu ndani. Ukiviacha nje bwana afya huvirarua na kuviharibu. Hii ilimaanisha ya kwamba nikilala ktk tent hili, basi nitakuwa zero distance na wenyeji wa huku (bwana afya na masikio). Siku hizi uwoga umepungua. Siku hii mimi nililisita kulala ktk hilo hema, ila kuna wadau wengine walilala ndani ya hilo tent na mengine ambayo yalikuwepo ktk camp.

Moja ya njia ambazo zinaelekea kwenye mjengo tuliolala sie ikitokea kwenye matent mengine makubwa na ofisi za camp. Unachokiona hapo kwenye njia ni nanihiiii ya tembo. Siku tulipofika ndovu camp (mida ya jioni), tuliambia kuwa masikio kadhaa walipita hapo kambini usiku wa kuamkia siku ile. unachokiona ni ushahidi wa ujio wao. Jikumbushe mtundiko kuhusu ndovu camp kwa ku-bofya hapa.

No comments:

Post a Comment