Monday, April 5, 2010

UDOM ilivyo sasa

Weekend ya pasaka, Team ya TembeaTz ilikuwa Dodoma kwa ajili ya 'conference'. Ikiwa huko team ilipiga tour ya fasta ndani ya UDOM na kujionea maendeleo ya chuo hiki.

Awali, Jengo la Chimwaga aka White house, ndio lilikuwa kielelezo cha chuo hiki. Lakini kwa sasa, Kuna vitu vingine vimeibuka na kuliweka kando jengo la Chimwaga ambako ndipo kilipoanzia chuo hiki. Chuo Kipo nje kidogo ya Manispaa ya Dodoma. Ni Chuo ambacho kina eneo kubwa la ardhi na sehemu kubwa ya eneo hilo lipo ktk mchakato wa kuendelezwa kwa namna moja au nyingine.


Ili kuokoa muda na pesa, Jamaa waliamua kufanya copy-and-paste kinamna ya mabweni ya Mabibo hostel na kwenda kuyaotesha UDOM. Kama unaelewa mabweni ya Mabibo hostel yalivyo, basi utaweza kuona mambo mawili matatu yanayoshabihiana. Kuiga mazuri sio kosa....

Kila kitengo kinajitegemea kwa madarasa, ofisi na hata mabweni ya wanafunzi wake. Zinaitwa Schools (kwa sie tuliokuwa UDSM zilikuwa zikiitwa Faculties kabla mfumo kubadilishwa). hapo UDOM, toka School moja kwenda nyingine kuna umbali kinamna. Ili kurahisisha mawasiliano, kuna mfumo mzuri wa barabara ambao tayari asilimia kubwa ipo ktk kiwango cha lami na taa zipo tayari kuangaza jua likizama. Ndani pia kuna mabasi (daladala) ambayo yanaweza kukutoa school moja kwenda nyingine. Kwa wenzangu na mie tuliokuwa UD, toka school moja kwenda nyingine ni kama kutoka iliyokuwa UCLAS kuja Utawala au Cafeteria. UDOM ni kubwa kieneo na ki-miundombinu!

Haya ni majengo ya School of Education; Kitengo kinachotarajiwa kubeba wanafunzi takriban 20,000. Hayo uyaonayo ni Mabweni ya wanafunzi wa school of Education.

Muendelezo wa majengo ya School of Education. Hapo kuna Mabweni, Madarasa na hata baadhi ya majengo ya ofisi.

Unaweza pata taarifa zaidi kupitia tovuti yao:
http://www.udom.ac.tz/

2 comments:

  1. SI MCHEZO! UDSM SASA ITAFUTE KWA KUJIFICHIA MAANA UDOM INATISHIA AMANI KWA STYLE HII.....

    ReplyDelete
  2. Majengo mazuri sana na panapendeza. Sasa wajitahidi wapande miti mingi. Sijaona mti hata mmoja hapo.

    ReplyDelete