Kila tarehe 10 ya mwezi wa Desemba ni siku inayotumika kuadhimisha tamko la kuheshimu na kulinda haki za binadamu duniani. kila kona ya dunia huwa kuna kuwa na hekaheka za kila namna ktk mchakato mzima wa kuazimisha siku hii. mwaka 2008 huko mjini Moshi, wanaharakati wa maswala ya haki za Binadamu waliamua kuadhimisha siku hii kwa style tufaoti kidogo. Walianza na maandamo ndani ya mji wa Moshi na kisha wakaendelea mbele zaidi na kwenda kulipandisha tamko la haki za binadamu ktk kilele cha mlima Kilimanjaro. Shughuli hii yote ilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ya tamko hili. Walifanya hivi ili kuonyesha dhana ya kwamba haki za binadamu zinatakiwa kulindwa, kuenziwa na kuinuliwa juu ili zieleweke kwa kila mmoja wetu. Picha juu ni mdau Rodrick (aliyeshika nembo iliyotumika kuashiria tamko hilo) akiwa sambamba na wanaharakati wenzie maeneo ya YMCA moshi kabla ya kuanza maandamano.
Maandamano ya wanaharakati yakipita mitaa ya moshi huku Kilele cha kibo kikionekana kwenye background.
Safari ya kuelekea kwenye kilele ca Afrika ikiendelea. hapa ni kipande kati ya Marangu gate na Mandara hut (point ya kwanza baada ya kupita Marangu gate).
Wanaharakati wakikatisha eneo lijulikanalo kama saddle. hapa ni eneo ambalo linachukua mandhari ya jangwa. Kwa mbali ni kilele cha Kibo ambako ndiko wadau walipokuwa wanaelekea
Japo walianza wengi lakini mwisho wa siku ni wachache ndio waliowawakilisha wenzao kwa kulifisha tamko hili Uhuru point, point ya juu kabisa ktk mlima Kilimanjaro. Baadhi ya wanaharakati hawakufanikiwa kufika kileleni kutokana na ukweli kwamba miili yao ilikumbana na changamoto za kimazingira na kushindwa kuendelea na safari.
Hili ni moja ya makundi au watu binafsi ambao huupanda mlima kwa malengo mengi mbalimbali, Ni vyema wadau tukijikusanya na kwenda kuupanda mlima kwa lengo moja tu (kwa kuanzia) nalo ni kuupanda mlima kuashiria uzalendo kwa taifa letu. Gharama ni nafuu kwa mzalendo ukilinganisha na gharama anazolipa mgeni asiye raia wa Jamhuri. Wasiliana na kampuni inayojishughulisha na kupeleka wageni kupanda mlima Kilimanjaro ili upewe mpango mzima wa jinsi safari inavyokuwa. Inaleta unafuu mkubwa endapo wapandaji mtakuwa ktk kundi lenye wapandaji zaidi ya 4. Ahsante ya picha kwa mdau Rodrick.

No comments:
Post a Comment