Wednesday, April 21, 2010

Mapito ndani ya hifadhi ya Lake Manyara NP

Kama kitu ambacho nchi yetu imebarikiwa ktk hifadhi zake ni upekee. Kila hifadhi iliyopo Tanzania ina upekee ukiilinganisha na hifadhi nyingine. Lake Manyara National park nayo ina upekee wa kuwa ni hifadhi ambayo uoto wake ni misitu. Hapa sehemu kubwa ya hifadhi ni msitu wenye mchanganyiko wa miti mbalimbali.

Mtundiko huu unajaribu kukuonyesha jinsi njia ambazo utakuwa unapita na gari ukiwa ktk game drive yako hifadhini. Unakuwa unapasua misitu huku ukikutana na wanyama mbalimbali njiani. Zaidi utawaona Tembo ambao ndio wa kumwaga hapa.

Ukiona kwenye picha unaweza usidhani kama upo hifadhini. Sheria na taratibu za safari za mbugani ni sharti uzizingatie ile kufanya safari yako kuwa ya furaha na salama. Kutokana na hali ya msitu wakati mwingine inakuwa ngumu kuwaona wanyama licha ya kwamba wapo.

Kuna sehemu unaweza ukafika ukakutana na wenyeji wameziba njia. situation kama hii haihitaji papara, itakulazimu uwe mdogo mpaka mwenyeji wako atakapoamua kukupisha au utafute njia nyingine ya kuendelea na safari yako.

No comments:

Post a Comment