Thursday, April 22, 2010

Hata tope humfaa...

Wadau, huu ni muendelezo wa lile swala la joto linalozalishwa tumboni kwa Bwana Afya wakati akimeng'enya chakula alichokula. Ukiachia wale bwana afya wa awali, hawa ni wengine ambao nao tuliwakuta Serengeti wakiwa ktk heka heka za kutuliza joto la mwili. Kuwakuta ktk tope, tena mahali ambapo ni wazi pasipo na kivuli ni ishara ya kwamba mateso ayapatayo kwa joto hilo ni makubwa kushinda kupigwa na jua kali la mchana.

Wameacha sehemu nyingine wamekuja kujichomeka sehemu ambayo kuna tope ili liwasaidie kulishusha joto la tumboni.

Huyu inaelekea alijipooza vya kutosha akawa ametoka nje ya tope kuanza kuangalia ustaarabu mwingine.

Uwepo wa marabou stork karibu na hawa mabwana afya ni ishara ya kwamba 'mabaki ya mzoga' haukuwa mbali na tulipowakuta hawa jamaa. Nasema mabaki ya mzoga nikiwa na maana ya kwamba hapo bwana afya kishachukua kila kitu na kilichobakia hapo si mali kitu tena.

unaweza jikumbusha kuhusu mtundiko wa awali kuhusu joto la mwili wa fisi kwa kubofya hapa. Fisi hawa, tuliwakuta sehemu mbili tofauti lakini wote wakiwa wanapambana na hali hii kwa style inayoshabihiana.

No comments:

Post a Comment