Wednesday, January 13, 2010

Safari za Majahazi ya Zanzibar

Unapokuwa mapumzikoni kisiwani Unguja, moja ya shughuli unayoweza kuifanya ukiwa huko ni kuzungukia maeneo kadhaa ya kisiwani humo (hasa hasa maeneo ya Kaskazini - Nungwi) kwa kutumia majahazi (dhow safaris). Majahazi yao ni salama na yanakuwa na life jackets ambazo unavaa muda wote wa safari

Mara nyingi Dhow trips huwa zinafanywa mida ya jioni

Raha huongezeka mkiwa wengi, kwani mnakuwa mnashindana. Mwanzoni nilikuwa na dhana ya kwamba haya Majahazi (kwa kuwa yanategemea upepo) basi daima yataenda upande ule tu ambao upepo unaelekea. lakini safari hizi za Majahazi zilinipa picha tofauti.

kwa kugeuza mkao wa tanga (kile kitambaa cheupe kikubwa), nahodha anaweza kubadili mwelekeo na kuelekea kokote kule anakotaka. hili jambo lilinishangaza lakini ndio ikawa kweli ya mambo. Challenge kubwa wanaipata endapo upepo utakuwa hauvumi, haupo. hapo jahazi linaweza simama au kuanza kusukumwa na maji.

Ukiwa ktk jahazi unapata fursa ya kuona mandhari ya hoteli zilizopo huko na baadhi ya sehemu utapita ktk pwani za vijiji vya wavuvi na kuona shughuli zinazoendelea kando kando ya bahari hindi.
Moja ya hoteli zinazopatikana ktk pwani ya Nungwi, jina limenitoka.

Hapa ni ktk pwani ya La Gemma Hotel. ukisikia mchanga wa pwani ndio huu, mweupe na laini kama poda

No comments:

Post a Comment