Thursday, April 15, 2010

Anapooza Injini

Porini, fisi hufahamika kama bwana Afya. Amepewa jina hili kutokana na tabia yake ya kula sehemu kubwa ya manyama na kuacha kidogo mno.
Inaelezwa ya kuwa mfumo wa mmeng'enyo (digestion system) wa fisi una acid/gastric juices kali sana (concentrated) hali ambayo inamuwezesha kusaga na kumeng'enya Mifupa, kwato na hata ngozi za wanyama anazokula. Mchakato mzima wa kumeng'enya hivi vitu huzalisha joto kali sana. Nadhani mliosoma kemia kwa Mkandawile au Mama Shija mtakumbuka mambo ya heat ktk reaction za chemistry. Fisi asipotafuta namna ya kulipooza joto linalotokana na mchakato huo, linaweza kumletea madhara mwilini mwake.
Ndio maana baada ya mlo na shughuli ya digestion ikipamba moto, fisi hupenda kukimbilia sehemu zenye maji au hata matope na kujitosa kama inavyoonekana ktk picha juu. Hii ni njia ya kuweza kumsaidia kupambana na joto litokanalo na mchakato unaoendelea tumboni mwake. Aghalabu si jambo la ajabu kumkuta fisi akiwa ametafuta hifadhi ktk dimbwi la maji hata kama ni machafu kupita maelezo.
Endapo maji ya kiwa adimu, basi hutafuta kivuli au pango ambalo litamkinga na jua na kisha atajificha humo mpaka hali itulie tumboni mwake. Hali hii pia inaelezea tabia ya fisi kupenda kuwinda usiku muda ambao joto la mazingira linakuwa limepungua ukilinganisha na mchana. Picha juu ni Bwana afya wawili wakiwa kando kando ya barabara ndani ya hifadhi ya Serengeti eneo la Seronera. Uwepo wao ktk hilo bwana ni dalili tosha ya kwamba wametoka kula kitu muda si mrefu.

1 comment:

  1. Niliwahi kusikia kwamba bwana afya anapoenda haja kubwa kwa bahati mbaya ikakumwagikia unaweza kuchubuka kama mtu aliyemwagiwa maji ya moto. Huu unaweza kuwa ushahidi kuwa joto linalotengenezwa katika mchakato huo wa kumeng'enya chakula chake ni la hali ya juu sana! Sina ushahidi.

    ReplyDelete