Wednesday, March 17, 2010

Wazee wa Mizoga wakizengea... Ngorongoro

Wadau wakiwa ktk pitapita zao ndani ya Ngorongoro kabla ya jua kuzama walikutana na huyo Pundamilia akiwa ametoka kuzaa mtoto muda si mrefu huku tayari mabwana afya wakimzengea mtoto wake. Mabwana Afya kwa kawaida wao zao ni mizoga, lakini wanapokutana na mnyama mdogo au aliyeumia huwa hawasiti kumdondosha na kuanza kujipatia msosi.

mwana Punda akiwa ananyonya maziwa huku bwana afya akiwa anakuna kichwa ili kupata mbinu yakuweza kunyakua toka kwa mama yake. Kwa mbali kidogo mbweha nao wanaonekana wakitafuta namna ya kufanya colabo/featuring na mabwana afya endapo dili lao likitiki!

Walikuwa wakijaribu kila namna kumchomoa huyo mtoto kwa mama yake ili waweza kuanza kumla. Zengwe hili lilihusisha fisi 3. Fisi wana tabia ya kuanza kumla mnyama kabla hata hajafa. wakishamdondosha, wote wanaachana na zoezi la kumuua na kuanza shughuli ya kumla. Simba na wengine, huuwa kwanza na kisha huanza kumla baadae.

Kuonyesha kuwa walikuwa hawatanii, waliamua kuweka kambi kabisa ili kusubiri muda muafaka (usiku) ili waweze kujitwalia mwana punda kiulaini. Kwa kuwa muda wa kuendelea kubaki crater ulikuwa unaelekea ukingoni, iliwalazimu wadau waachane na sakata hili na kuanza safari yao ya kutoka nje ya crater bila ya kujua hatima ya mwana punda.
Hivi ndivyo nature inavyo ji-balance yenyewe. Ukiingilia huu mfumo kwa kuiondoa jamii moja basi utavurga mfumo mzima na matokeo yake (mabaya) hayatachukua muda kujionyesha. Ahsante ya picha kwa wadau waliotembelea Ngorongoro na kushare na blog ya Tembeatz.

Mdau,
kama una picha za safari yako ya porini na ungependa kushare na wadau wengine kupitia blog ya TembeaTz, usisite kuzituma kupitia tembeatz@gmail.com nasi tutazipeleka hewani.

No comments:

Post a Comment