Wednesday, March 17, 2010

Zebra Point - Mlima Kilimanjaro

Wageni wanaokwea Mlima kilimanjaro kupitia route ya Marangu, wafikapo Horombo (moja ya vituo) wanakuwa na option ya kwenda kujionea mandhari ya kilele cha Mawenzi. Unapokuwa njiani kutoka Horombo kuelekea Mawenzi, unapita sehemu ijulikanayo kama Zebra point. Sehemu hii imepewa jina hili kutokana na hayo mawe kuwa na rangi mithili ya rangi ya pundamilia.
Option ya kwenda Mawenzi hutumika kwa manufaa ya kuuzoesha mwili mazingira ya huko juu - acclimatisation kabla ya kuendelea na safari kuelekea juu zaidi - Kibo point - ambako kuna upungufu zaidi wa hewa ya oksijen.

1 comment:

  1. Hapa Zebra point unakuta wapanda mliima wametengeneza viminara vya mawe (dragon)kama ishara ya kupata bahati njema ya kufika kilele cha Kibo. Kuwa mwangalifu usiangushe dragon ya mwnzako

    ReplyDelete