Wednesday, March 17, 2010

Lerai Forest, Ngorongoro crater

Huu 'msitu' unakutana nao ukiwa njiani kutoka Ngorongoro Crater - Crater ascent. Unaitwa Lerai Forest. Wengi huwa wanakuja huku kwa matumaini ya kumfuma wa juu (chui). Mandhari kama hizi zenye miti ndio maeneo anayopenda wa juu kujificha mida ya mchana.

Miti ya Acacia imeshika hatamu ndani ya huu 'msitu'.

Tembo nao huvinjari ndani ya Lerai forest.

Wengi hujenga picha ya kwamba Crater ni sehemu ya wazi. Ukweli ni kwamba ndani ya Ngorongoro crater kuna mandhari mbali mbali. kuanzia mabwawa, ukanda wa nyasi na hata misitu na kadhalika.

No comments:

Post a Comment