Sunday, March 7, 2010

Wageni walipoanza kumkwaza mwenyeji wao

Ni dhahiri kabisa kuendelea kuwepo kwa wadau pembezoni mwa hilo bwawa lenye viboko kulikuwa kumefika kikomo cha uvumilivu wa mmoja wa hao viboko. Hiyo hali ya kupanua mdomo kama unayoiona hapo juu ni ishara ya kwamba kiboko huyo amekerwa na 'wageni wake'. Kwa akili yake, yeye anahisi huu ni uvamizi ktk eneo lake jambo ambalo kiboko hupingana nalo kwa gharama yoyote. Hiyo ishara ya viboko ya kupanua mdomo ili kuashiria kutofurahishwa na mvamizi inaitwa THE GIANT GAPE. picha ilipigwa na wadau waliotembelea Seluos game Reserve

No comments:

Post a Comment