Hot Air Balloon Safaris (nadhani 'kimatumbi' yatakuwa yanaitwa mapulizo ya Moto) ni namna nyingine ambayo mgeni anaweza kutembelea hifadhi na kuangalia wanyama na mandhari ukiachia ile ya magari (Game Drive) ambayo imezoeleka toka enzi na enzi. Siku ya safari mpango mzima huwa unaanza alfajiri ambapo magari ya kampuni ya Serengeti balloon safaris humfuata mgeni ktk hotel/Campsite aliyofikia na kumleta eneo lijulikanalo kama Maasai Kopjes, sehemu ambayo safari za balloons huwa zinaanzia. Muda wa kuchukuliwa hotelini hutegemea umbali kati ya Hotel/Camp site uliyofikia na hapo Maasai Kopjes. Picha juu ni kikapu cha mojawapo ya maballoon ambacho kina uwezo wa kubeba abiria 8; kubwa linabeba abiria 16. mwanzoni kikapu kinakuwa kimelazwa kama kinavyoonekana. kazi ya hiyo feni pembezoni mwa kikapu inaonekana ktk picha ifuatayo.
Licha ya kwamba haya mapulizo yanahitaji hewa ya moto ili kuweza kuruka, kwa kuanzia huwa yanajazwa hewa ya baridi na mafeni yenye nguvu sana. Picha juu ni matokeo ya upepo mkali uliokuwa ukipulizwa na feni mbili wakati wa maandalizi ya puliza kwa ajili ya safari.
kwa kawaida kwa hawa jamaa wanakuwa wanarusha mapulizo mawili, lakini hii pia inategemea na idadi ya abiria. Siku ambayo kikosi cha Tembeatz kilifanya safari hii kulikuwa na mapulizo mawili. Linaloonekana juu ni pulizo pacha na tuliopanda sie ambalo hapo ndo ngoma inogile, safari kwishaanza...
Baada ya kulijaza hewa baridi kwa kiwango kinachostahili, Rubani huwasha Burners na kuanza kupasha moto hewa iliyopo ndani ya pulizo. Wakati huu abiria mnakuwa mpo tayari kwenye chemba zenu. mnakuwa mpo ktk position ya kulala. Hili pulizo lilikuwa na chemba 5; 4 za abiria-watu 2 ktk kila chemba; 1 ya pilot ambayo ipo katikati. Hewa ikipata moto, ndio hapo pulizo linapata uwezo wa kuruka na kuanza safari.
kwa jinsi ambavyo rubani anaendelea kupasha moto hewa na ndio jinsi pulizo linavyozidi kuamka na kukaa ktk up-right position ambayo imezoeleka kwa wengi. picha juu ni burners ambazo rubani hutumia kuweza kupashia moto hewa na kulipa balloon uwezo wa kuruka.
Ktk Mapulizo haya kuna mtandao wa kamba ambazo zinamsaidia rubani kuweza ku-control pulizo vizuri. kamba hizo zote zinakuja kuishia ktk chemba ya pilot (kamba nyekundu). ndani ya balloon kuna outlets ambazo rubani anazutimia anapotaka kaligeuza pulizo au kukata kona. akivuta kamba husika, outlet husika hufunguka na kuanza kuruhusu hewa ya moto kutoka nje kwa kasi na kisha kuleta effect ya kuligeuza balloon upande unaotakikana.
Moja ya vitu vilivotustaajabisha ni uwepo wa njia au vichochoro ndani ya mbuga ambavyo wanyama wanavifuata wafanyapo safari zao ndani ya hifadhi. Unapokuwa ktk gari unaweza kuona kuwa kama vile wanyama wanaenda hovyo hovyo, lakini ukweli ni kwamba wanyama nao wana njia zao ambazo zinaonekana ukiwa juu au ukiwa unafanya game walking. picha juu ni barabara kuu iendayo Musoma hadi Mwanza kutokea Arusha ambayo inakatisha ndani ya hifadhi ya Serengeti. Pembezoni mwa hiyo barabara kuna vichochoro vinavyoingia ktk manyasi, hiyo ndio mitaa yao wenyeji wa huko - wanyama pori.
Hapa rubani alilipeleka Balloon juu na kutupa mandari nzuri ya hifadhi. Eneo linaloonokena ni Seronera ambako kwa kiasi fulani miti imepata nafasi ya kushamiri. kwengineko ni nyasi mwanzo-mwisho.
Tulimkuta huyu nyati akiwa ndio nae anaamka; Rubani alitueleza kuwa huyu ni resident bull. akimaanisha yeye ni mkazi wa eneo hilo. mara kwa mara Balloon likipita mitaa hiyo yeye anakuwepo. Ukiachia u-resident, wengine huwa ni migratory (wanahama hama kusaka malisho na majike). Mnyama kuwa resident ni ishara ya kuzeeka.
Hapa ni baada ya kutua salama. Rubani alilishusha juu ya hilo trela moja kwa moja ili kuwarahisishia kazi mafundi ambao huwa na kazi ya kulisasambua baloon ili kulirudisha linakohifadhiwa na kuliandaa kwa safari ijayo. matundu pembezoni ya kikapu ni kwa ajili ya abiria kuweza kushukia baada ya safari. Picha juu ni fundi wa kampuni ya Serengeti Ballon Safaris akiendelea kulifungua balloon ili kulipeleka garage. Kwa ujumla safari za balloon huwa ni za saa moja ambapo mnaweza mkawa mtembea umbali wa takribani kilomita 15-20 ktk muda huo.
Mtundiko huu ni sehemu tu ya mambo ambayo mtu anayapata anapofanya balloon safaris. Mkitua salama, kinachofuata ni kitu kinaitwa Bush Breakfast - Staftahi ya porini. Kwa kuwa unakuwa umechukuliwa hotelini au camp site asubuhi sana, unakuwa unapatiwa kifungua kinywa baada ya safari. Stay tuneed......
Wakati wote wa safari yenu mnakuwa mnafuatwa na magari mawili - ground crew. moja lni a kubeba abiria baada ya flight na moja linakuwa na trela kwa ajili ya kulibebea balloon(Picha juu). Kila balloon inakuwa ground crew yake.
kuweza kupata mpango mzima wa balloon safaris wasiliana na tour operator aliye karibu nawe kwa taarifa kamili.
Wakati wote wa safari yenu mnakuwa mnafuatwa na magari mawili - ground crew. moja lni a kubeba abiria baada ya flight na moja linakuwa na trela kwa ajili ya kulibebea balloon(Picha juu). Kila balloon inakuwa ground crew yake.
kuweza kupata mpango mzima wa balloon safaris wasiliana na tour operator aliye karibu nawe kwa taarifa kamili.
No comments:
Post a Comment