Saturday, March 13, 2010

Game walking safari aka Makanyagio

Kwa wale wageni ambao hupendelea kusogea zaidi na karibu kabisa kwa wanyama, Selous game reserve inawapa nafasi ya kwenda hatua zaidi ya kuitembelea mbuga hiyo ukiwa ndani ya gari. Ukiwa Selous unaweza ukafanya Game walking safari. hapa mgeni unaachana na gari, na unaingia porini kwa miguu mkiwa sambamba na askari mwenye silaha (kama ilivyo hapo juu). Hii aina ya safari inampa mgeni nafasi ya kujifunza mengi mno.
Kiukweli, mambo mengi yanayohusu wanyama wa porini na mazingira yao huwa tunayakosa kwa kufanya 'ziara' zetu tukiwa ndani ya gari. Game walking inakuwa inakupeleka katika sehemu ambazo magari hayafiki na huko ndio unapokuta na hawa wanyama kwa ukaribu zaidi - japo wakati mwingine baadhi hukimbia kwa mshangao. ni katika game reserves na National parks chache (Arusha NP ikiwa ni Mojawapo) ambako game walking zinaruhusiwa. Ukiwa porini hizi safari hujulikana kama Makanyagio. Ahsante ya picha kwa mdau aliyekuwa sambamba na wanafunzi wa shule moja ya jijini waliopiga trip yao huko Selous hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment