Waswahili tunamuita Pofu. huyu mnyama ana ndugu yake ambae wenye lugha yao wanamuita Giant Eland; nadhani kwa kiswahili huyo atakuwa anaitwa Pofu mkubwa - sina uhakika.
Picha juu ni nje kidogo ya Ngorongoro crater ambako team ya TembeaTz ilimfuma pofu huyu akivinjari.
Kama kumbukumbu zangu ziko sahihi, niliwahi kusikia kwamba Pofu ana miiko yake kama ukitaka kumuwinda. nadhani kama tungepata wawindaji wangeweza kutuambia. Nilisikia kuwa ukitaka kumuwinda pofu siyo rahisi kihivyo, yaani si kama unavyoweza kuwinda digidigi au nyumbu na wengineo. Kuna ukweli???
ReplyDelete