Monday, March 1, 2010

Mnazi nao unatoa Fenicha!

Inaweza onekana kama ni utani lakini ukweli wa mambo ni kwamba gogo la Mnazi linatoa mbao nzuri na tena ngumu mno ambazo zinaweza kutumika kutengenezea samani (fenicha) kwa matumizi mbalimbali. Tembeatz ilibahatika kutembelea moja ya viwanda vilivyopo nje kidogo ya Jiji ambavyo vinashughulika na utengenezaji wa bidhaa mbalimbali za ndani kwa kutumia magogo ya mnazi. Picha juu ni shehena ya mbao za mnazi ambazo zinasubiri kuingia ktk mkondo wa uzalishaji. Msimamzi wa kiwanda hicho aliitonya TembeaTz kwamba shehena hii ya magogo inatoka Zenj kwakuwa huko ndio kuna minazi mizuri kwa fenicha. Mnazi mzee (miaka 80 kwenda mbele) ndio unatoa mbao bora.
hizi ni sehemu ya kitanda kinachotokana na mbao ya mnazi. Kwa sasa consigment hii ni kwa ajili ya Hoteli moja ambayo ipo ktk mchakato wa mwisho wa ujenzi. ki ukweli bidhaa hizi hata maskani zinafaa pia.

Makabati ya jikoni

Frames za madirisha

hii nayo ni frame ya dirisha ikiwa imepigwa pini kisawasawa.

Dressing table ikiwa ktk hatua za mwisho kiwandani kabla haijakamilika na kuingia sokoni.

Park benches an viti kwa ajili ya dressing tables na matumizi mbalimbali vinatengenezwa kwa mbao za mnazi pia.
Makabati ya Nguo nayo pia

Kutokana na ubao wa mnazi kuwa mgumu, uunganishwaji wa fenicha unafanya kwa kutumia hivi vidubwasha (mafundi wanaviita doweli). Msumari unadunda na kupinda. najua wengi watabisha lakini ukweli ni kwamba, unapopiga msumari ktk mnazi (ambao haujakatwa au kutolewa magamba ya pembeni) unakutana na magamba ambayo ni laini. na hivyo kufanya msumari wako kupenya kiulaini. lakini magamba ya nje ya kitolewa na ukabakia na ile sehemu ya ndani, basi utajikuta umebakia na ubao ambao utakupa shida kupigilia msumari.

Sehem ua shehena za dressing tables ambazo zipo ktk mchakato kiwandani hapo.

No comments:

Post a Comment