Licha ya Kwamba Saadani NP ndio mbuga ambayo ipo karibu zaidi na Dar, ukweli unabakia kuwa Mikumi ndio mbuga inayofikika kirahisi zaidi (kwa barabara) toka Dar. Mdau AM alikuwa huko ametumwagia taswizar zifuatazo ili nasi tujionee yale aliyoshuhudia ktk safari yake hiyo. Picha juu ni Thompson Gazelles, hao wenye pembe ni madume. wakiwa ktk kundi namna hii kundi hilo linaicha bachelor's group. Kundi la majike huwa na dume mmoja tu mwenye pembe ambae ndio anakuwa mtawala wa kundi hilo. Bachelors wao kazi yao ni kujifua ili siku moja wakapamba na dume mwenye kumiliki kundi ili wampindue na kisha mmoja wao achukue himaya.
Wa juu (chui) alionekena akiendelea na shughuli zake za kila siku pembeni ya kiji-bwawa kidogo. Ni dhahiri alikuwa ametega mingo hapo ili apate kujitwalia mnyama atakae kuja kunywa maji hapo.
Yangeyange wakiwa wametanda pembezoni mwa hippo pool ya mikumi. hii ni sehemu maarufu sana kwa wageni kwenda na kupata lunch wakiwa ktk mizunguko yao ndani ya Mikumi NP.
Combination ya usalama; kipindi ambacho nyasi zinakuwa ndefu. ushirikiano kama huu (Twiga na pundamilia) unaimarisha usalama wa wanyama. Twiga kwa urefu wake anaweza kumuona adui tokea mbali na kuashiria hatari kwa wengine ili kukimbia na kuokoa maisha yao.
Nyati wakioga tope karibu kabisa na Mikumi wildlife camp (Vibanda unavyoviona kwa nyuma). hapo ndio Mjengwa alitembelewa na wenyeji wake - Sharubu aka Simba.
Kujipaka tope ni namna moja ya wanyama kupambana na wadudu wanaowatambaa ktk ngozi yao na pia ni namna ya kupambana na joto. Hapo kama kuna kupea au wadudu wengine, tope hilo hupelekea wadudu hao kufa na kumfanya mnyama kuendelea kuishi bila kero yao. wale ambao wata-survive tope, basi nyati huwa na uswahiba na ndege wengine ambao hutua na kuwaondoa wadudu hao. ni ushirikiano ambao wanao wanyama ili kunusuru maisha yao.
Jamani, hata simba jika anaitwa sharubu?.Au mimi ndiye sijui?
ReplyDeleteporini simba wote ni sharubu,haijalishi ni jike au dume,jina lina heshima yake hilo
ReplyDelete